Mpya Lake Zone Camp Meeting Soma zaidi
Global Family Gatherings

Kuhusu Sisi

Mtume Shemeji Melayeki
Mtume Shemeji MelayekiMwanzilishi na Msimamizi wa Huduma

Historia Yetu

Huduma ya Global Family Gatherings ilianzishwa mwaka 2016 na Mtume Shemeji Melayeki, ikilenga kufundisha mafundisho sahihi (sound doctrine) ili kuwakuza waamini kufikia ukomavu na kuufikia ulimwengu kwa ufunuo wa Kristo katika Maandiko.

Tunafundisha Neno la Mungu kwa njia ya kimfumo ya kutafsiri Maandiko. Lengo letu kuu ni kufuata mpango wa Mungu kwa kuhubiri Injili na kufanya wanafunzi — ili kila mtu, kila mahali afikiwe na kuimarishwa katika kweli, na kuwa watu imara wanaotimiza mapenzi ya Mungu duniani.

Huduma kwa sasa inafikia mikoa mingi ya Tanzania — ikiwemo Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mwanza, Dodoma, Singida, Mbeya, Ruvuma, Geita, Kigoma, Manyara, Shinyanga na Zanzibar — pamoja na Eswatini. Makao makuu ya ibada yako Dar es Salaam, katika ukumbi wa Dar Social Hall, Sinza Lego, Barabara ya Shekilango.

God’s Standards

Tunachoamini na kukiishi

Maono Yetu

Viwango na vielelezo vya Kimungu (watu wa Neno, Maombi na Roho) kupitia Uinjilisti, Mafundisho, Ibada, Ushirika, na kufanya kazi kama Familia ya Waamini.

Jiunge na Kanisa

Jiunge na Kanisa Letu

Asante kwa nia yako ya kujiunga na kanisa letu.

Tafadhali jaza fomu kwa kuchagua mkoa wako na kuweka taarifa zako. Tutatumia taarifa hizi kukuunganisha na tawi la kanisa lililo karibu nawe, na kukusaidia unapokuwa sehemu ya jamii yetu.

Tunatarajia kukukaribisha na kutembea pamoja nawe katika safari yako ya kiroho.

Pakua