Global Family Gatherings Tabata imeanza rasmi

Kwa neema ya Mungu, huduma ya Global Family Gatherings Church — Tabata imeanza rasmi.
Kama uko maeneo ya karibu, chakula kimekufikia karibu sasa — maeneo ya Tabata.
Kipekee nikukaribishe kwenye kusanyiko hili Jumapili hii. Uhakika ni kwamba utapata muda wa kutosha kuomba na kujifunza.
- Utafundishwa kuomba na kuelekezwa. Siyo tu kuomba, ila kuomba sawasawa na maagizo ya kimaandiko na kuomba katika Roho. Kama hujawahi kunena kwa lugha, utasaidiwa pia.
- Utapata muda wa kujifunza Neno la Mungu kwa muda wa kutosha, tena kwa uchambuzi wa maandiko — siyo maneno ya mtaani na breaking news. Utafundishwa kwa utaratibu (systematically) kwa ushahidi mwingi wa maandiko.
- Utahudumiwa na kujifunza kuwahudumia wengine.
- Utaandaliwa kujua Neno la Kweli na kufundishwa hatua kwa hatua namna ya kuwafikia wengine.
KAMA UNATAFUTA KANISA LA AINA HIYO pale Tabata, basi umepata. Karibu sana Global Family Gatherings Tabata!
Ratiba na mahali
Mahali: Kinyerezi, St. Rosalia Primary School
- Ijumaa – Maombi: Garden Street, Kinyerezi · saa 3:00 usiku hadi 11:00 alfajiri (21:00 – 05:00)
- Jumapili – Ibada ya Jumapili: St. Rosalia · saa 3:00 asubuhi hadi 7:00 mchana (09:00 – 13:00)
Mchungaji: Pastor Benedict Mallya – +255 764 196 390